Job 28

Mapumziko: Imani Inakopatikana


1 a“Kuna machimbo ya fedha,
na mahali dhahabu isafishwapo.

2 bChuma hupatikana ardhini,
nayo shaba huyeyushwa kutoka mawe ya madini.

3 cMwanadamu hukomesha giza;
huyatafuta hadi sehemu iliyo mbali,
kwa ajili ya kuchimbua mawe yenye madini
katika giza jeusi sana.

4 dHuchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu,
mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu;
mbali na wanadamu huning’inia na kupembea kwa kamba.

5 eArdhi, ambako chakula hutoka,
chini hugeuzwa kwa moto;

6 fyakuti samawi hutoka katika miamba yake,
nalo vumbi lake lina vipande vya dhahabu.

7 gHakuna ndege awindaye aijuaye njia ile iliyofichika,
wala hakuna jicho la mwewe lililoiona.

8 hWanyama wa porini wanaotamba hawajawahi kupakanyaga,
wala simba azungukaye huko.

9 iMikono ya mwanadamu hushambulia miamba migumu sana,
na kuiacha wazi mizizi ya milima.

10 jHutoboa shimo refu la kupenya chini kwa chini kwenye miamba;
macho yake huona hazina zake zote.

11 kHutafuta vyanzo vya mito
na kuvileta vitu vilivyofichika katika nuru.


12 l“Lakini hekima inaweza kupatikana wapi?
Ufahamu unakaa wapi?

13 mMwanadamu hatambui thamani yake;
haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai.

14 Kilindi husema, ‘Haiko ndani yangu’;
bahari nayo husema, ‘Haiko pamoja nami.’

15 nHaiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi kuliko zote,
wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha.

16 Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri,
kwa shohamu ya thamani kubwa au yakuti samawi ya thamani kubwa.

17 oDhahabu wala mawe maangavu haviwezi kulinganishwa nayo,
wala haiwezi hubadilishwa na vito vya dhahabu.

18 Marijani na yaspi hazistahili kutajwa;
thamani ya hekima ni zaidi ya akiki nyekundu.

19 pYakuti manjano ipatikanayo Kushi haiwezi kulinganishwa nayo,
wala haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi.


20 “Ni wapi basi hekima itokako?
Ufahamu hukaa wapi?

21 qImefichika machoni pa kila kitu kilicho hai,
imesitiriwa hata kwa ndege wa angani.

22 rUharibifu na Mauti husema,
‘Ni uvumi wake tu uliotufikia masikioni mwetu.’

23 sMungu anaifahamu njia ya kuiendea hekima
na ndiye peke yake anayefahamu inakokaa,

24 tkwa maana yeye huitazama miisho ya dunia
na huona kila kitu chini ya mbingu.

25 uAlipofanyiza nguvu za upepo
na kuyapima maji,

26 valipofanya maagizo kwa ajili ya mvua
na njia kwa ajili ya umeme wa radi,

27 ndipo alipoitazama hekima na kuikadiria thamani yake,
akaithibitisha na kuihakikisha.

28 wNaye Mungu akamwambia mwanadamu,
‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima,
nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ ”
Copyright information for SwhKC